Kuhusu familia

Tovuti hii ni mamlaka ya wanafamilia wote waliokwenye familia ya marehemu mzee Benedict Chonya wa Malangali, Iringa iliyoanzishwa kwa lengo la kupeana taarifa za muhimu zinazohusu familia zikiwemo taarifa za matatizo kama misiba, magonjwa na taarifa za sherehe mbalimbali za wanafamilia hii zikiwemo shughuli za Harusi, send-off, kipaimara, sherehe za mikutano ya kifamilia hususani vikao vya kila mwaka.

Na ikumbukwe kwamba familia iliyo na umoja ndio yenye mafanikio, tusaidiane kwa pamoja kuinua umoja wetu kwa kuchangia michango yetu ya kila mwezi.
Katika umoja huu tumeweka kiwango kidogo cha kuchangia kila mwanafamilia, utatakiwa kuchangia Tshs 2000/= tu kila mwezi ili kuinua mfuko wa umoja wetu. Tumeamua kuanza na kiwango hicho kwa kila mwezi kwani tunaimani asilimia kubwa ya wanafamilia ni wanafunzi hivyo tumeweka kiwango hicho ili kila mmoja aweze kumudu kuchangia.

Pia tumeamua kufungua mtandao huu (Blog) wa wanafamilia ambao utakuwa unatoa taarifa za kila matukio yanayohusu familia hii. Hususani kuna taarifa ambazo ni zakufahamishana kwa mfano; kuna mugonjwa, kifo, harusi na zote ambazo zitakuwa up to date kwenye mtandao huu ukiachilia mbali kwa njia ya simu.

Kutakuwa na tarehe ya kukutana ambayo itapangwa na mwenyekiti, muweka hazina na mtunza data. Hiyo itakuwa tayari baada ya kukaa na kuona kuwa uwezekano wa kukutana na mfuko wetu unaweza ku'manage, hivyo basi taarifa zitatolewa na kukutana tarehe na siku iliyopangwa.....kwa baadhi ya mapendekezo ya baadhi ya wanafamilia walipendekeza iwe kila mwisho wa mwaka.

Asante!
KAULI MBIU YETU
"MAFANIKIO YAANZE NDANI YA FAMILIA"


No comments:

Post a Comment